Watoto 394 hubakwa kila mwezi Tanzania

WatotoOngezeko kubwa la matukio ya ubakaji wa watoto ni mara tatu zaidi ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2017

BBC Swahili

Ripoti iliyotolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania imebainisha kwamba kuna ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya watoto kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza katika mwaka 2018.

Ongezeko kubwa la matukio ya ubakaji wa watoto ni mara tatu zaidi ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2017, kutoka 12 kwa mwaka hadi 533 kwa mwaka 2018.

Hivyo ni wastani wa watoto 394 wamebakwa kila mwezi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania bara kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2018.

Fundikira Wazambi ambaye ni ni afisa programu msaidizi dawati la utafiti katika Kituo cha sheria na haki za binadamu akielezea hali ya ukatili ameeleza kwamba watoto waliobakwa ni asilimia 66 huku wanawake ni asilimia 34,hivyo ripoti hiyo imebainishwa kwamba kuna idadi kuwa wa watoto unyanyasaji ya watoto.

Takwimu zinaonesha mara nyingi mbakaji ni mtu wa karibu wa familia ambaye anaweza kuwa mjomba, kaka wa shangazi hadi wafanya kazi wa Nyumbani( shamba boy ).

Mtoto anadaiwa kuwa ni rahisi zaidi kubakwa nyumbani zaidi ya sehemu yeyote ile.

Adhabu ya viboko yasababisha kifo cha mwanafunzi Tanzania

Wakati huohuo ndoa za utotoni na ukeketaji zimedaiwa kuwa changamoto kubwa kwa watoto.

Huku kwa upande wa wanawake, ukatili wa kimwili na ukatili wa kingono kuna wastani wa wanawake 203 wamebakwa kila mwezi katika kipindi cha Januari hadi Juni 2018.

Ukatili wa dhidi ya wanawake hadi kupelekea mauti hasa unasababishwa na wivu wa kimapenzi ,wengi huwa wanachomwa moto ,kupigwa na vtu vyenye ncha kali na kuuwawa kikatili.

Ripoti hiyo imeeleza pia kuwa kuna muonekano wa kuimarika kidogo kwa haki ya kuishi kwa mwaka 2018 ukilinganisha na mwaka jana.

Mauaji yanayotokana na imani za kishirikina yamepungua kutoka 172 hadi 106,ambapo watu 172 hadi 106 wanauwawa kutokana na imani za kishirikina,wakisemwa wachawi.

Na hakujaripotiwa matukio ya kuuwawa kwa walemavu wa ngozi ingawa bado wanaishi kwa hofu.

SAMA PIA: Ubakaji mjini Kisii, polisi wasaka washukiwa