Tattoo mpya ya msanii Diamond yazua maswali miongoni mwa mashabiki

Diamond Platinumz

Mwanamuziki Diamond Platinumz amechora tattoo mpya mkononi mwake na imeibua maneno mengi miongoni mwa mashabiki.

Mashabiki wengi wanajiuliza kujiuliza ni kwa Diamond kajiongezea tattoo wakati tayari anazo nyingi kwenye mwili wake.

Tattoo hiyo ambayo ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii kuanzia Jumanne, iliacha gumzo zaidi kutokana na mwonekano wake na herufi zilizokuwepo katika tattoo hizo.

Baadhi ya watu wanahisi kuwa ni herufi zinazowakilisha mianzo ya majina ya watoto wake.

Tattoo hiyo ina herufi N, D, T, N na asemekana kuwa ni majina ya watoto wake watatu Nillan, Dylan , Tifaah na jina lake yeye mwenyewe.

Je, unapenda kuisikiliza miziki mikali ya Kiafrika? Bonyeza hapa.