Sarah Cohen adai DCI fidia ya shilingi milioni 500

Sarah Wairimu Cohen anadai idara ya upelelezi DCI inafaa kumfidia shilingi milioni 500.

Sarah Wairimu ambaye ni mshukiwa mkuu katika mauaji ya mumewe Tob Cohen anadai kwamba fidia hiyo itagharamia uharibifu na nyumba yake iliyoko katika eneo la Kitisiru.

Sarah Cohen amedai kuwa idara ya Uchunguzi DCI imemzuia kutumia mali yake kinyume na sheria.

Siku ya Jumatano, hakimu Lydia Achode alisema kuwa sharti angesikiliza pande zote mbili kwanza. Hakimu Achode aliweka Januari 15 kuwa tarehe ya kusikiliza upande wa mshtakiwa na mshtaki.

Idara ya uchunguzi ilizuia Nyumba yake katika eneo la Kitisuru baada ya mwili wa marehemu Tob Cohen kupatikana katika shimo moja nyumbani kwake.

Tangu siku hiyo mjane Sarah Wairimu ameingia katika mvutano na idara ya DCI kuhusu kumzuia kuingia au kutumia nyumba hiyo wakisema kuwa hilo ni eneo la uchunguzi.

Awali, Sarah Cohen aliwasilisha maombi kadhaa kuingia nyumbani mwake kuchukua nguo na gari lake, vitu ambavyo wakili wake anasema havihusiani na kesi hiyo.

Wachunguzi wamepinga vikali ombi la Saraha Wairimu wakisema kuwa uchunguzi bado unaendelea katika eneo hilo, kwa hivyo hangekubaliwa kuingia na kutumia nyumba yake.

PIA SOMA: Mkuu wa shambulizi la kigaidi Wajir alikuwa mwalimu wa eneo hilo