Raia Mkenya awasili Zimbabwe kwa kesi ya kuupinga ushindi wa Mnangagwa

Zimbabwe Emmerson Mnangagwa.Rais wa Zimbabwe

Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change (MDC) kimetafuta huduma za wakili ambaye ni raia wa humu nchini Edgar Otumba Ouko, kukiwakilisha katika kesi ya kuupinga ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa.

Ouko amabye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Maseno, atasaidia kubaini iwapo kulikuwa na dosari kwenye matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Julai 31, 2018 nchini humo, ambapo Mnangagwa alitangazwa mshindi.

Kwa mujibu wa chama cha upinzani chini ya uongozi wa Chamisa, kulikuwa na dosari wakati wa kuhesabu kuria na kuathiri matokeo ya mwisho, na kwamba kura zilihesabiwa mara mbilimbili na madai hayo ndiyo yanayotegemewa na mrengo huo katika kesi yake.

Rais Mnangagwa aidha, anasema alishinda uchaguzi huo kwa njia huru na haki na kwamba madai ya upinzani hayana msingi wowote.

Comments are closed.