Msiendelee kunizuilia gerezani, nastahili kuwa na mwanangu, Maribe ajitetea

maribe

Mwanahabari Jacque Maribe ameiomba mahakama imwachilie kwa dhamana kwa kuwa hana mume na anastahili kuwa na mwanawe mwenye umri wa miaka minne.

Maribe ambaye ametupwa rumande kwa wiki nyingine baada ya mahakama kuahirisha kesi yake hadi Oktoba 24, aliandika hati ya kiapo kuiomba mahakama dhamana hiyo kwa madai kuwa mwanawe ni mdogo na mwenyewe hana mume.

“Mimi sijaolewa na nina mwanangu mdogo mwenye umri wa miaka 4 anayenitegemea kwa hali na mali. Bado ni mdogo na huenda akapata shida nyingi iwapo nitaendelea kuwekwa rumande hadi mwisho wa kesi hii ambayo inaweza kuchukua muda mrefu,”alieleza.

Ikiwa unapenda kuisikiliza miziki mikali ya kiafrika bonyeza hapa.

Jacque aliiambia mahakama kuwa hawezi kwenda kinyume na taratibu za kuachiliwa kwa dhamana kwa kuwa ni mtangazaji maarufu na Wakenya wengi wanamjua. Aliiomba mahakama kumwachilia kwa dhamana ili awe na mwanawe ambaye huenda akawa anateseka kisaikolojia.

“Hakuna kizuizi chochote kinachoweza kufanya nisipate dhamana. Mimi ni mwanahabari maarufu wa runinga. Wakenya wengi wananijua na kufahamu kazi yangu na popote niendapo najulikana na jambo hili lanifanya nisithubutu kwenda kinyume na taratibu za kuachiliwa kwa dhamana. Sikuhusika kwa njia yoyote na mauaji, na sikuwa katika sehemu yalikofanyika mauaji hayo wala sikumjua Monica. Lawama zozote zinazoelekezwa kwangu kuhusu mauaji hayo ni kutokana na kosa langu la kumpenda Irungu,”Jacque aliongeza.

PIA SOMA: Dadake Jacque, Cathylene Maribe amliwaza kwa masaibu anayopitia