Mourinho mwishowe azungumza baada ya United kushindwa Shire Kuli na Brighton

MourinhoKocha wa Man United Jose Mourinho.

Kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho, amekubali kuwa wachezaji wake walifanya makosa wakati wa mchuano dhidi ya Brighton & Hove Albion ambayo yalifanya timu hiyo kushindwa kwa mara ya kwanza katika msimu.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea alisema hilo alipokuwa akijibu maswali ya wanahabari ambao walimuuliza kilichoendelea uwanjani.

“Tulifanya makosa na tuliadhibiwa na makosa hayo,” na kumpuzilia mbali mwanahabari huyo alipomuuliza kuhusiana na ushirikiano wa wachezaji uwanjani.

Mchuano huo ulikuwa katika uwanja wa Amex, Jumapili Agosti 19. Man U ilishinda Leicester City 2-1 katika mchuano wa kufungua msimu uwanjani Old Trafford ambapo Paul Pogba na Luke Shaw waliipa timu hiyo ushindi waliostahili.

Be the first to comment on "Mourinho mwishowe azungumza baada ya United kushindwa Shire Kuli na Brighton"

Leave a comment

Your email address will not be published.