Matiang’i aikaribisha familia ya aliyekuwa mwanajeshi Josphat Nuru ofisini kwake

Matiang'i

Waziri wa usalama Dkt. Fred Matiang’i ameikaribisha familia ya aliyekuwa mwanajeshi Josphat Nuru katika ofisi yake siku ya Ijumaa ambapo aliwafariji na kuwatia moyo.

Matiang’i alipozitembelea afisi za polisi wa kupambana na ghasia GSU aliwapongeza maafisa wote na wale waliowajibika kwa haraka wakati wa shambulizi la kigaidi Dusit2 14 Riverside, Nairobi.

Waziri aliongoza dakika moja ya utulivu kwa heshima za mwendazake.

Aidha, alitoa ujumbe wa pongezi kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta  kwa polisi waliowajibika wakati wa shambulizi.

“Rais amenituma nije kuwaambia jinsi anavyojivunia kitengo hiki cha polisi. Tunajivunia kama taifa, serikali na huu ni ujumbe kwa ulimwengu kwamba taifa hili lina wake kwa waume wanaojitolea kusaidia nchi yao kila wanapohitajika,” alisema Matiang’i.

Akiwahutubia wajumbe kutoka mataifa ya kigeni, waziri wa masuala za kigeni Monica Juma alisema shambulizi hilo la kigaidi halikulenga taifa la Kenya tu, ila dunia nzima.

“Ingawa shambulizi hili lilifanyika katika hoteli ya Dusit2 hapa nchini, lililenga dunia nzima. Hoteli hiyo inafanya kazi na kutoa huduma kwa watu wengi humu duniani,” alisema.

Sikiliza Radio Halisi kwa kubonyeza hapa.