Khaligraph Jones amzawidi meneja wake na gari jipya

KhaligraphMsanii Khaligraph Jone (kulia) akimpokeza meneja wake funguo za gari alilompa kama zawadi ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Rapa wa mziki wa hiphop almaarufu Khaligraph Jones ameisisimua mitandao ya kijamii baada ya kumtunuku meneja wake gari la kifahari katika sherehe za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Jones alisema yeye na meneja wake wamekuwa marafiki wa kufaana na kwa muda mrefu na hakuwa na budi ila kumunulia gari kama njia moja ya kipekee ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

“Leo ningependa kumpatia rafiki yangu zawadi ya shukran kwa juhudi zote alizoziweka kwa taaluma yangu ya muziki, tangu siku zile tukiwa katika shule ya upili tulikuwa na ndoto ya kufanikiwa maishani na kwa kweli Mungu ametubariki kwa sasa,” Papa Jones alisema huku akimkabidhi meneja wake Shire Kuli ufunguo wa gari.

Wafuasi wake mitandaoni walifurahishwa na kitendo hicho na ukarimu wake huku wengine wao wakimhimiza aendelee kuwa na moyo huo wa kutoa.

Be the first to comment on "Khaligraph Jones amzawidi meneja wake na gari jipya"

Leave a comment

Your email address will not be published.