Hazina ya kitaifa kuzuia fedha kwa kaunti kumi na tano

Hazina ya kitaifa imeliomba bunge la kitaifa kuidhinisha uamuzi wake wa kuzuia kutolewa kwa fedha takriban shilingi bilioni 22.5 kwa kaunti kumi na tano kutokana na madeni ambayo hayajashughulikiwa.

Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi aliagiza kamati ya kuratibu bajeti (Budget Appropriations Committee) kuangazia kwa haraka ombi la hazina ya kitaifa.

Wafanyabiashara wamedai kuwa idara za kitaifa na zile za kaunti zimechelewa malipo ya kima cha shilingi bilioni 150 na kuwalazimisha kurudia kazi za viwango vya chini ili kuwakimu.

“Nimeagiza kamati hiyo kuchunguza na kujua iwapo kaimu Waziri Ukur Yatani aliafikia agizo la kipengee cha usimamizi wa fedha za umma (PFM) alipoomba bunge hili kuzuia fedha kwa kaunti zilizoathirika na kuripoti kwa muda unaohitajika,” Muturi alisema alipotuma ujumbe kuhusu ombi hilo la Ukur Yatani kwa wabunge.

Sheria inahitaji hazina ya kitaifa kutafuta uidhinishaji kabla ya kusimamisha kutolewa au kugawa fedha kwa kaunti.

Hazina ya kitaifa imetaja kaunti kumi na tano zinazoadhibiwa baada ya kukosa kukamilisha ulipaji wa madeni katika notisi iliyotolewa Novemba 22.

Kaunti hizo ni Narok,Machakos, Nairobi, Vihiga, Isiolo, Tana River, Migori, Tharaka Nithi, Bomet, Kirinyaga, Nandi, Mombasa, Kiambu, Garissa, na Baringo.

Kaunti hizo kumi na tano zimefeli kulipa ada zinazohitajika kuanzia mwezi wa Julai na Oktoba, jambo lililosababisha hazina ya kitaifa kuzuia fedha kuelekezwa kwa kaunti hizo.

Kusoma habari zetu katika lugha ya Kiingereza bonyeza hapa.