Bahati na Yvette Obura hawakomi kugombana licha ya kila mmoja Yvette kuolewa kwingine

Yvette

Kuwepo kwa Diana Marua kama mkewe Bahati kunazidi kuzua ugumu  baina ya  mwanamuziki huyu na Yvette Obura ambao wanajizatiti  kumlea mtoto wao Mueni Bahati.

Akizungumza wakati alipohojiwa katika kipindi cha Reality TV Show ‘Being Bahati’, Yvette alisema mara nyingi hugombana na Bahati kwa kuwa baina yao hakuna anayetaka kusikiliza mwingine.

“Co-parenting si rahisi, you know he has a wife halafu may be am in another relationship. Halafu unajua kuna zile time hatuwezi pigiana pigiana simu ati Mueni anataka hii. Sisi wote ni vichwa ngumu, tunakuwanga na arguments, every now and then the main focus ni Mueni, sisi ni non-foctor,” Yvette alieleza.

Bi Obura alisema sababu iliyomfanya kutosikizana na baba mtoto ni kuwa alitaka kumfunza mtoto Kiingereza ilhali yeye na mwanawe wanaishi maeneo ya Eastlands ambako lugha ya mawasiliano ni Kiswahili.

“Huko Instagram unaeka picha ya Mueni watu wanauliza kwani haendangi shule, baba yake at ooh mtoto hanafaa kujua English, mi siongeangi English, so mi nilidecied to kucall the Dad so atakuwa anamchukua yeye mwenyewe huko Eastlands anampleka mpaka Runda, labda Mueni atatoka huko na Pizza tutakula pia sisi,” Yvette alieleza.