Ali Kiba na Ommy Dimpoz hawana sifa – Shamsa Ford

Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania, Shamsa Ford amesema wanamuziki Ali Kiba na Ommy Dimpoz hawana sifa za kuwa watu wanaopaswa kumwoa, kwa kuwa hawana sifa.

Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI, kinachorushwa kwenye kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, ambapo amesema kwa sasa bado anatamani kuolewa hajakoma na akitokea mwanaume mwenye nia hiyo atakubali bila kusita.

“Ni kweli matamani kuolewa hata sijakoma na Mungu inshallah atanipa mume, ila kwa sasa sitaki kufanya makosa tena,nikiwa kama mtoto wakike nataka niwe mfano bora kwa wasichana wanaoniangalia, ikitokea kesho Mungu akinipa mume sahihi naiolewa sijakoma.”

“Kati ya Ali Kiba, Marioo, na Ommy Dimpoz hakuna hata mmoja mwenye sifa za kuwa mume wangu” ameongeza Shamsa Ford.

Hivi karibuni msanii huyo wa Maigizo alisema, kutokana na uzuri alio nao, anaamini mwanaume anayetaka kumwoa kwa sasa anapaswa kutoa mahari ya shilingi Milioni 20.

PIA SOMA: Tattoo mpya ya msanii Diamond yazua maswali miongoni mwa mashabiki